Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake yamaliza semina mbili na imeanza kusajili washiriki wa semina nyingine ya Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kukamilika semina mbili ya (Almawadah) na (Abulfadhil) za ufundishaji wa hukumu za usomaji wa Quráni na tahfiidh kwa wanawake, baada ya kukamilisha ratiba waliyo andaliwa na kufanya mitihani ya kuhitimu semina hizo.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa Maahadi bibi Manaarah Jaburi amesema: “Ni muendelezo wa semina za Quráni zinazo fanywa na Maahadi ndani ya mwaka huu, na kwa mujibu wa mkakati ulio andaliwa kwa ajili ya mwaka huu, kila semina ilikua na masomo maalum kulingana na kiwango cha elimu za washiriki na umri wao, jumla ya washiriki kumi wamehifadhi Quráni kupitia semina ya Almawadah, huku washiriki kumi na tisa wakihitimu semina ya hukumu za usomaji wa Quráni, semina hizo zimefanywa chini ya wakufunzi wa kike walio bobea katika fani ya Quráni”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya kuhitimisha semina hizo mbili Maahadi imeanza kusajili washiriki wa semina nyingine maalum kwa mabinti wa Najafu wenye umri tofauti, miongoni mwa masomo watakayo fundishwa ni: (kisomo sahihi, hukumu za usomaji, kuhifadhi Quráni tukufu), semina itafanywa kwa njia ya mtandao, kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba za simu zifuatazo: (07601887952 – 07601887951) au (07601887951) kupitia telegram”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: