Ugeni kutoka wakfu Sunni umetembelea maktaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu na kuonyesha nia ya kuimarisha ushirikiano wa kielimu na kimaarifa baina yao

Maoni katika picha
Mkuu wa kituo cha nakala-kale na uhuishaji wa turathi katika uongozi wa wakfu Sunni Dokta Dhiyaau Abdu-Latifu Al-Maríy, ameonyesha nia ya kuimarisha ushirikiano wa kielimu na kimaarifa pamoja na maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na kubadilishana uzowefu baina ya pande mbili kwa ajili ya kuboresha sekta ya maktaba, hususan katika kuhuisha turathi na kutunza nakala-kale pamoja na kuzifanyia matengenezo.

Yamesemwa hayo katika ziara iliyofanywa na ugueni huo kwenye kituo cha maktaba na daru makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, sehemu ya kwanza wametembelea kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi, wamepokelewa na mkuu wa kituo hicho, Ustadh Swalahu Siraji aliye waonyesha vitengo vyote vya kituo na kueleza kazi ya kila kitengo.

Kisha ugeni ukaelekea katika kituo cha kukarabati nakala-kale na utunzaji wake, kiongozi wa idara hiyo Ustadh Liith Lutfi akaeleza kwa kina kazi zinazo fanywa na kituo, baadhi ya shughuli alizielezea na kuzionyesha kwa vitendo, kisha wakaonyeshwa nakala za Quráni zilizo andikwa karne tofauti za hijiriyya na namna ya utunzwaji wake kwa kutumia njia mpya zinazo endana na teknolojia ya kisasa.

Mwisho wa ziara hiyo ugeni umetoa shukrani kwa mapokezi mazuri waliyo pewa, na wakaonyesha kuridhishwa na mambo waliyo ona katika ziara hii, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kisasa vinavyo tumika upigaji picha nakala kale na faharasi au ukarabati, pande mbili zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika mambo ya kielimu na kimaarifa kwa lengo la kubadilishana uzowefu, ukizingatia kuwa kituo cha ukarabati wa nakala-kale cha Atabatu Abbasiyya tukufu kina uzowefu mkubwa katika sekta hiyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: