Idara ya Quráni tukufu imetangaza kuanza usajili wa wanafunzi watakao hifadhi Quráni tukufu

Maoni katika picha
Idara ya Quráni chini ya ofisi ya maelekezo ya Dini tawi la wanawake, linalo fungamana na ofisi ya katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuanza kwa usajili wa tahfiidh-Quráni na hukumu za usomaji.

Masharti ya muombaji:

  • 1- Awe na cheti cha sekondari (upili) na kuendelea.
  • 2- Asiwe na umri wa chini ya miaka (18) na sio zaidi ya (25).
  • 3- Asiwe ni mwanafunzi wa shule ya msingi.

Masomo yatafundishwa kwa njia ya mtandao, mitihani itafanywa kwa kuhudhuria moja kwa moja ndani ya Atabatu Abbasiyya, kila baada ya kuhifadhi juzuu tano, aidha mshiriki anatakiwa kuwa tayali kufanya mitihani midogo midogo itakayo tolewa kila mara kwa njia ya mtandao.

Mwisho wa usajili ni tarehe (10/03/2021m).

Kumbuka kuwa idara ya Quráni inalenga kuboresha kiwango cha elimu ya Quráni kwa wanawake wa kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: