Idara ya ustawi wa jamii inafanya kazi kubwa kutokana na tahadhari za kujikinga na maambukizi

Maoni katika picha
Idara ya ustawi wa jamii chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeongeza utendaji kazi wa idara yake na mawakibu zilizo chini yake, kutokana na tahadhari mpya iliyotangazwa ya kujilinda na maambukizi ya virusi vya Korona, huu ni muendelezo wa kazi kubwa waliyofanya siku za nyuma na kuendeleza uwepo wake kila wakati na kila mahala.

Kiongozi wa idara Sayyid Qassim Maámuriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mawakibu za kutoa misaada zilizopo mikoani zenye uhusiano na idara ya ustawi wa jamii ya Atabatu Abbasiyya tukufu, zinatengeneza misafara ya kusaidia kwenye kila mkoa, zitaendesha opresheni ya kupuliza dawa na kugawa chakula kwa familia za mafakiri na mayatima katika mikoa yote ya Iraq, kufuatia kuanza kwa marufuku mpya ya kutembea”.

Akaongeza kuwa: “Ofisi za idara yetu kwa kushirikiana na mawakibu wanazo fanya nazo kazi, zimekusudia kushirikiana na kikosi kazi kilichoundwa na serikali za vitongoji, pamoja na kikosi cha ulinzi wa taifa na mamlaka zingine zinazo shiriki kwenye vita ya kupambana na kuenea kwa virusi vya Korona”.

Maamuriy akasisitiza kuwa: “Idara (19) na mamia ya mawakibu kutoka mikoa tofauti kuanzia kaskazini hadi kusini na kwa kushirikiana na wahisani pamoja na wadau tofauti wanao fanyia kazi fatwa ya kusaidiana kijamii, wameandaa kiwango kikubwa cha vifaa-tiba na mitungi ya gezi za kusaidia upumuaji, sambamba na mamia ya vifurushi vya chakula kwa lengo la kusambaza kwa wanaostahiki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: