Ugeni kutoka chuo kikuu cha Diyala unaangalia namna ya kushirikiana na maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya

Maoni katika picha
Ugeni kutoka chuo kikuu cha Diyala/ kitivo cha masomo ya kiislamu ukiongozwa na mkuu wa taaluma Dokta Fadhili Ahmadi Hussein, umetembelea kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi na kituo cha ukarabati wa nakala-kale chini ya maktaba na Daru-Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na chumba maalum cha kutunzia nakala-kale.

Ugeni huo umepokewa na mkuu wa kituo cha upigaji picha nakala-kale na faharasi Ustadh Swalahu Siraji ambaye ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Hakika hii ni moja ya ziara nyingi zinazo fanywa na viongozi wa sekula waliobobea katika mambo ya maktaba, kituo cha kwanza cha ugeni huo kilikua kituo chetu, ambapo wameangalia utendaji wa kazi na vifaa vinavyo tumika, tumetoa maelezo kamili ya kila kitengo”.

Akaongeza kuwa: “Baada ya hapo tukaenda katika kituo cha kukarabati nakala-kale, tukapokelewa na mkuu wa kituo hicho Ustadh Liith Lutfi, aliukaribisha ugeni na kuutembeza katika korido za kituo pamoja na kueleza kazi kubwa wanazo fanya, na nakala-kale walizo zifanyia ukarabati ambazo historia yake inarudi nyuma kwa miongo mingi tofauti, hali kadhalika ugeni umeonyeshwa vifaa vinavyo tumika na kuwaonyesha chumba cha kutunzia nakala-kale adim”.

Akafafanua kuwa: “Ugeni umeonyesha kufurahishwa na utendaji wa vituo ulivyo tembelea, na umeonyesha nia ya kushirikiana na kubadilishana uzowefu baina ya pande mbili, hususan katika mambo yanayo husiana na turathi za nakala-kale, kwa kufanya kila jambo la lazima katika kuendeleza elimu hiyo tukufu, kwa faida na maendeleo ya taaluma ya sekula, na kufanya kazi zinazo changia kukuza sekta hii na kunufaika nayo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: