Mwezi kumi Rajabu Aswabu kwa umma wa kiislamu na wafuasi wa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), ni siku ya kukumbuka kuzaliwa kwa nuru ya tisa miongoni mwa nuru za Maimamu waongofu, naye ni Imamu Muhammad Aljawaad (a.s), aliyekuwa anasubiriwa kwa hamu kubwa na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), Imamu huyu alikua kilele cha utukufu na ukarimu kwa wapenzi na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), alizaliwa mwaka wa 195h.
Imamu Aljawaad, jina lake kamili ni: Muhammad bun Ali bun Mussa bun Jafari bun Muhammad bun Ali bun Hussein bun Ali bun Abu Twalib (a.s), mama yake ni bibi Sakina Marziyya na inasemekana ni Khaizarani, na mke wake ni bibi Sumana kutoka Moroko, Imamu alikua kilele cha utukufu na ukarimu kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) na wapenzi wao.
Katika kitabu cha (Manaqibu Aali Abu Twalib) cha ibun Shahru-Aashubu imeandikwa kuwa, bibi Hakimah bint Abu Hassan Mussa bun Jafari amesimulia namna alivyo zaliwa, na karama zilizo tokea, anasema: Ummu Abu Jafari (a.s) alipo karibia kujifungua, Imamu Ridhwa (a.s) aliniita, akasema: (Ewe Hakimah nenda kahudhurie mazazi yake), akaniingiza ndani, akatuwashia taa na akafunga mlango.
Baada ya kuzaliwa nilimlea miguuni, Imamu Ridhwa (a.s) akaja, akafungua mlango na akamchukua (a.s) na kumuweka miguuni kwake kisha akaniambia: (ewe Hakimah mtikise-tikise) ilipo fika siku ya tatu, aliangalia mbunguni (a.s) halafu akaangalia upande wa kulia na kushoto kisha akasema: (Nashuhudia hakuna Mola ispokua Allah na hakika Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu).
Nikasimama kwa hofu nikamfuata Abulhassan (a.s) na kumuambia: nimesikia jambo la ajabu kwa huyu mtoto, akasema (a.s): (kitu gani)? Nikamuamia. Akasema (a.s): (ewe Hakimah utaona maajabu mengi kwake).
Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) alizaliwa mwezi kumi Rajabu mwaka wa (195h), jina lake ni (Muhammad), na kuniya yake ni (Abu Jafari).
Kuzaliwa kwake kulileta furaha kubwa kwa wafuasi wake na kuliongeza imami katika nyoyo zao, na kuondoa shaka iliyokua imeingia katika nyoyo za baadhi yao.
Imamu Muhammad Aljawaad (a.s) alikulia katika nyumba ya Utume na Uimamu, nyumba ambayo Mwenyezi Mungu ameitukuza, alipata malezi mema ya baba yake Imamu Ridhwa (a.s), alisimamia yeye mwenyewe malezi ya mwanae, alikuwa anatembea pamoja naye nyumbani na safarini hadi akakuwa (a.s), alipata elimu kubwa kutoka kwa baba yake (a.s), hadi akawa na uwezo mkubwa wa kufundisha wanachuoni elimu mbalimbali, na akawahimiza kuandika mambo aliyokua anawafundisha kutoka kwa baba zake watakatifu.
Miongoni mwa majina na sifa zake (a.s) ni: (Aljawaad, Attaqi, Azzaki, Alqaanii, Almurtadhwa, Muntajab) na mashuhuri zaidi ni (Aljawaad) kutokana na wingi wa utoaji wake na upole wake, akawa anaitwa (Baabu-Muraad), kutokana na wingi wa kusaidia kwake shida za watu, muda wa uhai wake (a.s) ni miaka (25) na Uimamu mika (17).