Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inafungua semina mpya za Quráni

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imefungua semina tatu mpya za Quráni, ambazo ni: (semina ya Ajyaal) na (Twayibaat) na (Muhsinaat), muendelezo wa mradi wa Quráni unaolenga kufundisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni kwa jamii ya wanawake.

Kiongozi wa Maahadi bibi Manaarah Jaburi amesema kuwa: “Semina hizi zinalenga wasichana wenye umri tofauti katika jamii, semina ya Ajyaal inawanafunzi (15) wenye umri kati ya miaka (8 -12), nao wanafundishwa kuhifadhi Quráni tukufu, na semina ya (Muhsinaat na Twayibaat) wanafundishwa hukumu za usomaji wa Quráni na kila moja inawanafunzi (20), huku semina ya (Muhsinaat) ikilenga wanafunzi wa sekula”.

Akaongeza kuwa: “Semina hizi zinafundishwa kwa njia ya mtandao chini ya walimu wenye uwezo mkubwa, kutokana na janga la korona linalo sumbua taifa kwa sasa”.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inalenga kufundisha elimu ya Dini kwa wanawake, na kipaombele chake yakiwa ni masomo yanayo husu Quráni tukufu, na kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wa Quráni wenye uwezo wa kufanya tafiti za kielimu katika mambo yote yanayo husu Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: