Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imekamilisha ratiba ya tafsiri ya Quráni ya kila wiki (visa bora), iliyohusisha utoaji wa mihadhara ya kuelezea visa vyilivyomo ndani ya Quráni.
Ratiba hiyo imeendeshwa na Shekh Ali Akili katika mkoa wa Najafu, amefafanua aya kutoka sura tofauti ndani ya Quráni tukufu.
Tambua kuwa tahadhari zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona yalizingatiwa wakati wa ratiba hiyo, ikiwa ni pamoja na umbali kati ya mtu na mtu na uvaaji wa barakoa.
Kumbuka kuwa ratiba hii ni sehemu ya harakati zinazo fanywa na Maahadi, chini ya mfululizo wa harakati zinazo husu Quráni, kwa lengo la kueneza utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu katika jamii.