Ugeni kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetoa pole kwa familia za mashahidi wa shambulio la kigaidi katika kitongoji cha Khaniqina na umechukua jukumu la kugharamia matimabu ya majeruhi

Maoni katika picha
Ujumbe kutoka Atabatu Abbasiyya tukufu umetembelea mkoa wa Dhiqaar, na kutoa pole kwa familia za mashahidi wa Hashdu-Shaábi na kutembelea majeruhi, walio pata shahada na wengine kujeruhiwa wakati wakizuwia shambulio la kigaidi lililofanywa na mabaki ya maharamia wa Daesh, kaskazini ya kitongoji cha Khaniqina katika mkoa wa Diyala siku chache zilizo pita.

Ugeni huo umeongozwa na Sayyid Adnani Jalukhani Mussawi kutoka kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Ziara hii imetokana na maenekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, ili kuja kutoa pole na kuziliwaza familia za mashahidi wa Dhiqaar, waliopata shahada wakati wanapambana kulinda taifa hili tukufu lisije kunajisiwa na magaidi wa Daesh, pamoja na kutembelea watu waliojeruhiwa kwenye shambulio la makao makuu ya mkoa wa Dhiqaar pamoja na vijijini na kuangalia hali yao, na kupongeza ushujaa walio onyesha wakati wa kuzuwia shambulizi la magaidi wa Daesh katika kitongoji cha Khaniqina”.

Akaongeza kuwa: “Hii sio ziara ya kwanza, tumesha fanya ziara nyingi tangu ilipotolewa fatwa takatifu ya kujilinda, iliyo tolewa na Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, hili ni jambo dogo sana tunalo weza kuzifanyia familia hizi zilizo jitolea wapenzi wao watukufu, kwani sisi tunaishi kutokana na utukufu wa damu zao na kujitolea kwao, tumewafikishia rambirambi za watumishi wa Atabatu Abbasiyya wakiongozwa na kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu awape subira wanafamilia wa mashahidi na awaponye haraka majeruhi”.

Akamaliza kwa kusema: “Ziara hii imepewa umuhimu mkubwa na familia za mashahidi na majeruhi, wametoa shukrani nyingi na kusema kuwa imepunguza machungu ya msiba”.

Sayyid Muhammad Hashim Muhammad Ali kiongozi wa taasisi ya Alfadhil ya kulea mayatima tawi la mkoa wa Dhiqaar, aliye fuatana na ugeni katika kutenbelea familia hizo amesema kuwa: “Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kwa kushirikiana na hospitali ya rufaa Alkafeel tutagharamia matibabu ya majeruhi na mahitaji ya lazima katika mchakato wa tiba”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: