Eneo la katikati ya haram mbili takatifu linafanyiwa usafi na kupuliziwa dawa

Maoni katika picha
Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya opresheni kubwa ya kusafisha na kupuliza dawa katika uwanja wa katikati ya malalo mawili matakatifu la Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona ulio anza kutekelezwa hivi karibuni kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi hivyo, opresheni hii inasaidia kulinda usalama wa mazuwaru na watumishi, pia wametumia nafasi ya kutokuwepo kwa watu katika eneo hilo kutokana na marufuku ya kutembea iliyo wekwa hivi karibuni hapa mkoani kwa ajili ya kujikinga na maambukizi.

Rais wa kitengo hicho Sayyid Naafii Mussawi amesema: “Opresheni hii ni muendelezo wa opresheni nyingi tulizo fanya siku za nyuma, kwa kuzingatia maelekezo yanayo tolewa na idara ya madaktari katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kamati ya kujikinga na maambukizi, imehusisha eneo la nje linalo zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hadi katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu, wakamalizia katika eneo lililopauliwa na maeneo yanayo zunguka uwanja huo, kwa kutumia dawa zinazo tengenezwa na shirika la Khairul-Juud zilizo thibitishwa ubora wake”.

Kumbuka kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu imeimarisha uchukuaji wa tahadhari za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, na inatekeleza maelekezo yote ya kujikinga na maambukizi kama yalivyo tolewa na mamlaka zinazo husika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: