Ustadh wa visomo vya mashairi kutoka nchini misri amepongeza miradi ya Maahadi ya Quráni tukufu amesema ni mizuri inastahiki pongezi

Maoni katika picha
Ustadh wa visomo vya mashairi kutoka nchini Misri Muhammad Fahami Abdu Sayyid Usfuur amepongeza miradi ya Quráni inayo fanywa na Maahadi ya Quráni tukufu, chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, akasema kuwa ni mizuri inastahiki pongezi.

Ameyasema hayo alipo tembelea Maahadi ya Quráni tukufu na kupokelewa na mkuu wa Maahadi Shekh Jawadi Nasrawi, Usfuru akaambiwa shughuli zinazo fanywa na Maahadi ya Quráni ikiwa ni pamoja na uchapishaji wa msahafu mtukufu, pamoja na usomeshaji wa Quráni, tahfiidh na tafiti mbalimbali kuhusu Quráni pamoja na mipango ya baadae, kwa lengo ya kuhamasisha kufanyia kazi mafundisho ya Quráni katika jamii, wakazungumzia mambo tofauti yanayo husu namna ya kuboresha zaidi huduma zinazo tolewa na Maahadi ya Quráni.

Mwisho wa ziara hiyo Usfuru akawataka waendelee kufanya kila wawezalo kwa ajili ya Quráni tukufu katika kutumikia vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitakatifu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: