Kuadhimisha mwaka wa saba tangu kuanzishwa kwake: kituo cha turathi za Hilla ni moja ya vituo kumi vya turathi

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu, ni kituo cha kumi cha turathi, kinaadhimisha mwaka wa saba tangu kuanzishwa kwake.

Hafla imefanywa ndani ya ukumbi wa kituo na kutolewa mhadhara wenye anuani isemayo: (Shekh Waramu Alhilliy na mchango wake kielimu), mtoa mada alikua ni Dokta Hussein Alfatliy.

Baada ya mhadhara kulikuwa na michango mabalimbali ya maoni pamoja na maswali yaliyo elekezwa kwa mhadhiri, naye alijibu na kufafanua zaidi pale palipohitajika ufafanuzi.

Hafla imepambwa na kaswida kutoka kwa mshairi Swalahu Lubani, ameimba kuhusu hilla ya zamani na turathi za wanachuoni wake, baada ya kaswida hiyo ndio ukafunguliwa mlango wa maswali na majibu kuhusu turathi za Hilla na wanachuoni wake wakubwa.

Kumbuka kuwa kituo cha turathi za Hilla ni moja ya vituo vilivyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na kinafanya kazi kubwa ya kuhuisha turathi za Hilla, ikiwa ni pamoja na kuchapisha vitabu na harakati zingine mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: