Mradi wa jengo la shule la kwanza na tatu limepiga hatua kubwa ya ukamilishwaji

Maoni katika picha
Kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimepiga maeneleo makubwa katika ujenzi wa jengo la shule la kwanza na la tatu katika eneo la mtaa wa Maálaji, mafundi wanaojenga mradi huo wamekamilisha kazi kwa kiwango kikubwa.

Tumeongea na rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi Mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh kuhusu swala hilo, amesema kuwa: “Kazi inaenda vizuri chini ya shirika linalotekeleza mradi huo, wanatarajia kukamilisha ujenzi ndani ya muda uliopangwa, hakika Atabatu Abbasiyya tukufu inafuatilia kwa karibu ujenzi huo na kutatua changamoto za kiutendaji”.

Mhandisi mkazi wa mradi huo Ali Hamidi amesema kuwa: “kiwango cha ukamilifu ni zaidi ya asilimia (%80), hatua za ukamilishaji zinazo endelea ni pamoja na kupaka rangi, kuweka vioo kwenye madirisha, na uwekaji wa umeme umekamilika kwa asilimia (%80) huku mambo mengine yakikaribia kukamilika”.

Akabainisha kuwa: “Kazi inaendelea vizuri, mradi huu unatarajiwa kuwa na matokeo mazuri baada ya kukamilika kwake, kwani unamitambo ya kisasa inayosaidia usomaji kwa njia nyepesi”.

Kuhusu hatua ya pili, Mhandisi Saadi Rahimu mkuu wa shirika la Albaladawi linalo tekeleza mradi huo amesema kuwa: “Hatua ya pili ya mradi imehusisha kazi maalum za ujenzi wa chini, kazi hizo zimesha kamilika kwa kiwango za asilimia (%45), ikiwa ni pamoja na kuweka lami na kusawazisha sehemu za njia pamoja na kujenga mitalo (mifereji) ya maji, sambamba na kazi ya kuweka taa na kufunga kamera za ulinzi, wakati huo huo kazi ya kufanyia uchunguzi vifaa vya umeme inaendelea”.

Tambua kuwa Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kazi kubwa ya kuporesha harakati za malezi na elimu hapa mkoani, kwa kufungua shule mbalimbali na kuboresha mazingira ya usomaji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: