Mwezi kumi na tatu Rajabu ni siku aliyozaliwa simba wa Mwenyezi Mungu mwenye kushinda na wasii wa Mtume wake Ali bun Abu Twalib (a.s)

Maoni katika picha
Ulimwengu umenawirika, giza limeisha, tawala za matwaghuti zimetetemeka, siku kama ya leo mwezi kumi na tatu Rajabu mwaka wa thelathini tangu kutokea tukio la watu wa tembo, na mwaka wa ishirini na tatu kabla ya kuhama (hijrah), ilizaliwa Quráni itamkayo, mbora wa mawasii na kiongozi wa waumini Ali bun Abu Twalib (a.s), malaika wakapeana habari njema ya kuzaliwa kwake na ardhi ikanawirika kwa nuru yake, alizaliwa (a.s) ndani ya Kaaba takatifu, hakuwahi kuzaliwa kabla yake wala hatazaliwa baada yake humo mtu yeyote, ni utukufu mkubwa ambao Mwenyezi Mungu amempa na kuonyesha ukubwa wa heshima yake.

Mazazi matukufu:

Kutoka kwa Said bun Jubairi anasema: Yazidi bun Qaánab anasema: Nilikua nimekaa na Abbasi bun Abdulmutwalib pamoja na kundi la Abdul-Uza pembeni ya nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, akaja Fatuma bint Asadi mama wa kiongozi wa waumini (a.s) alikua na ujauzito wa miezi tisa, akiwa ameshapata uchungu, akasema: Ewe Mola mimi ninakuamini, na ninaamini mafundisho yako kutoka kwa motume na vitabu vyako, ninaamini maneno ya babu yangu Ibrahim, aliyejenga nyumba hii, naapa kwa haki ya aliyejenga nyumba hii na mtoto aliyepo tumboni kwangu unifanyie wepesi uzaaji wangu.

Yazidi bun Qa’nab akasema: Tukaona nyumba imejifungua na Fatuma akaingua na kutoweka machoni mwetu kisha ukuta ukajifunga, tukaenda kufungua mlango lakini haukufunguka, takatambua kuwa jambo hilo ni amri ya Mwenyezi Mungu mtukufu, akatoka baada ya siku nne akiwa amemshika kiongozi wa waumini (a.s) kisha akasema: Mimi nimetukuzwa pamoja na wanawake wema waliotangulia kabla yangu, alitukuzwa Asiya bint Muzahim kwa sababu alimuabudu Mwenyezi Mungu kwa siri sehemu ambayo hatakiwi kuabudiwa Mwenyezi Mungu na yeyote mwenye kumuabudu anapata madhara, na Maryam bint Imran alitikisa mtende mkavu ukadondosha tende nzuri zilizoiva, na mimi nimeingia katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na nimekula matunda ya peponi, nilipotaka kutoaka nimesikia sauti ikiniambia: (Ewe Fatuma mwite Ali, huyo ni Ali, na Mwenyezi Mungu na mkuu, mimi nimetoa jina lake katika jina langu, na nimemuadabisha adabu zangu, na nimemuwezesha kupata sehemu ya elimu yangu, huyo ndiye atakayevunja masanabu katika nyumba yangu, na ataadhini juu ya nyumba yangu, atanitakasa na kunitukuza, amefaulu atakae mpenda na kumtii, na ole wake atakae mchukia na kumuasi).

Kuniya na laqabu zake:

Kiongozi wa waumini Ali (a.s) analaqabu na kuniya pamoja na sifa nyingi, ni vigumu kutaja zote, zimetoka kwa Mtume (s.a.w.w) kwenye matukio tofauti aliyo shiriki (a.s) katika kutangaza uislamu na kumlinda Mtume.

Miongoni mwa laqabu zake (a.s) ni:

Kiongozi wa waumini, pambo la Dini na waislamu, kiboko wa shirki na washirikina, muuwaji wa makafiri na wasaliti, kiongozi wa waumini, mfananishwa na Haruna, mridhiwa, nafsi ya Mtume na ndugu yake, mume wa Batuli, Upanga mkali wa Mwenyezi Mungu, kiongozi wa watu wema, muuwaji wa waovu, mgawaji wa pepo na moto, mbeba bendera, bwana wa waarabu, mshona kandambili, mtatuzi wa shida, mkweli mkubwa, mwenye pembe mbili, muongoaji, mpambanuzi, mlinganiaji, mwenye kushuhudia, mlango wa mji, walii, wasii, mlipaji wa madeni ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, mtekelezaji wa ahadi zake, habari kubwa, njia iliyo nyooka…

Miongoni mwa kuniya zake ni:

Abu Hassan, Abu Hussein, Abu Sibtaini, Abu Rihanaini, Abu Turaab.

Kiongozi wa waumini (a.s) amemtumikia Mwenyezi Mungu maisha yake yote, maisha yake yalianzia katika nyumba takatifu ya Mwenyezi Mungu na yakaishia katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, hakika maisha yake yote yalikua ni jihadi na kumtumikia Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: