Balozi wa Indonesia nchini Iraq amesema kuwa: Ziara yangu katika makumbusho ya Alkafeel ni jambo tukufu katika maisha yangu

Maoni katika picha
Balozi wa Indonesia nchini Iraq Maru Lobizi ametembelea makumbusho ya Alkafeel katika Atabatu Abbasiyya tukufu, na ameangalia korido za makumbusho akiwa pamoja na viongozi wa makumbusho, na kuangalia maendelea yaliyopo katika makumbusho hiyo yanayo endana na usasa wa maonyesho na utunzaji wa malikale, akasikiliza maelezo kutoka kwa wahifadhi wa makumbusho, ambao walifafanua namna ya uonyeshaji na utunzaji wa malikale.

Lobizi amefurahishwa na mpangilio wa makumbusho hiyo pamoja na malikale nadra alizo ziona, akasema kuwa: “Napenda kutoa shukrani za dhati kwa kupata fursa ya kutembelea sehemu hii tukufu, hakika hii ni sehemu nzuri yenye historia kubwa, nina furaha sana kutembelea mahala hapa, hiki ni kituo kitukufu zaidi ambacho nimebahatika kutembelea katika uhai wangu, natoa pongezi na shukrani kwa watumishi na wasimamizi wote walio saidia kufanikiwa ziara hii”.

Kumbuka kuwa makumbusho ya Alkafeel hupokea wageni na viongozi kutoka mataifa mbalimbali, kufuatia maendeleo makubwa yanayo shuhudiwa katika makumbusho hiyo, sambamba na malikale ilizo nazo, kupatikana kwa ziara hizo kunaifanya kuwa na sifa ya kimataifa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: