Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la Hindiyya inatangaza kuanza usajili wa semina mpya

Maoni katika picha
Maahadi ya Quráni tukufu/ tawi la hindiyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kuanza usajili wa semina itakayo fanyika kwa njia ya mtandao yenye jina la (Baswaairu Qurániyyah).

Semina hiyo itafanywa kwa njia ya telegram itakuwa na masomo yafuatayo (hukumu za usomaji, tahfiidh na maarifa ya Quráni), semina itaanza mwanzoni mwa mwezi wa Shabani 1442h, kwa wanaopenda kushiriki wawasiliane nasi kwa namba za simu zifuatazo:

📞 07602328941
📞 07725416647
📞 07830062965

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni katika Atabatu Abbasiyya tukufu na matawi yake yote yaliyopo mikoani, inalipa kipaombele sana swala la kuendesha semina za Quráni pamoja na warsha, mihadhara na harakati zingine zinazo imarisha utamaduni wa kufanyia kazi mafundisho ya Quráni tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: