Kuanza kwa shindano la wanawake la kuhifadhi na kusoma khutuba ya bibi Zainabu (a.s) katika kikao cha Yazidi (maluuni)

Maoni katika picha
Shindano la wanawake linalo endeshwa kwa njia ya mtandao la kuhifadhi na kusoma khutuba ya bibi Zainabu (a.s) katika kikao cha Yazidi (laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake), linalo simamiwa na idara ya wahadhiri wa Husseiniyya chini ya Atabatu Abbasiyya, khutuba iliyo mtetemesha maluuni huyo, inayo anza kwa kusema: (Kila sifa njema anastahiki Mola wa walimwengu, na rehema na amani ziwe juu ya Mtume wake na kizazi chake chema, kisha mwisho wa waliofanya uovu ni mbaya, wamekadhibisha aya za Mwenyezi Mungu na wakawa wanazifanyia shele…, hivi ulidhani ewe Yazidi baada ya kututembeza kama wanavyo tembezwa watumwa kuwa tutadhalilika mbele ya Mwenyezi Mungu na wewe utapata utukufu?!...).

Bibi Taghridi Tamimi makamo kiongozi wa idara hiyo amesema: “Shindano hili ni sehemu ya kukumbuka kifo cha bibi Zainabu (a.s) mwezi kumi na tano Rajabu, na kuchangia kusambaza turathi halisi za Maimamu wa Ahlulbait (a.s), na kuendeleza kauli tukufu aliyo sema bibi Zainabu (a.s), isemayo: (Wallahi hautafuta utajo wetu), sambamba na kuonyesha nafasi yake (a.s) na khutuba hii ni moja ya vielezi vyake”.

Akaongeza kuwa: “Wasichana wenye umri tofauti wanaruhusiwa kushiriki kwenye shindano hili, na litaendeshwa kwa njia ya mtandao”.

Akasisitiza kuwa: “Kuna zawadi watakazo pewa watakao faulu kama ifuatavyo:

Mshindi wa kwanza: dinari laki mbili (200,000).

Mshindi wa pili: dinari laki moja na elfu hamsini (150,000).

Mshindi wa tatu: dinari laki moja (100,000).

Washiriki wote pia watapewa zawadi ya Abaa (baibui)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: