Huzuni imetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na kuomboleza kifo cha Aqilah bani Hashim (a.s).

Maoni katika picha
Siku kama ya leo mwezi kumi na tano Rajabu, ni siku ya kumbukumbu inayo umiza na kuhuzunisha watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w), nayo ni kumbukumbu ya kufariki kwa Aqilah bani Hashim bibi Zainabu (a.s), aliye fariki siku kama ya leo mwaka wa 62 hijiriyya katika mji wa Damaskas Sham.

Katika kuomboleza msiba huu, haram ya kaka yake Abulfadhil Abbasi (a.s) imewekwa mapambo meusi, na alama za majonzi na huzuni zimetanda, pamoja na kuandaa ratiba ya kuomboleza inayo endana na mazingira ya sasa kiafya, kuna ratiba inayo endeshwa kwa njia ya mtandao na mahudhurio, aidha kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeweka ratiba ya kupokea mawakibu za waombolezaji zitakazo miminika katika malalo takatifu, mwaka huu kutakua na mawakibu chache zitakazo wasilisha mawakibu za watu wa Karbala, kutokana na marufuku ya kutembea iliyopo.

Kumbuka kuwa bibi Zainabu (a.s) alifariki mwezi (15) Rajabu mwaka wa (62h), baada ya jina lake kuingizwa katika wanawake watakatifu, wafuasi wa Ahlulbait (a.s) hufanya majlisi za kuomboleza kila mwaka wakati wa kumbukumbu hii.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: