Kitengo cha Dini kinaratibu mhadhara wa Dini kuhuisha kumbukumbu ya kifo cha shujaa wa Karbala bibi Zainabu (a.s)

Maoni katika picha
Katika kuomboleza kifo cha Aqilah Twalibina bibi Zainabu Kubra mtoto wa kiongozi wa Waumini (a.s), kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu kinaendesha ratiba ya kutoa mihadhara ya kidini ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), asubuhi ya siku ya mwezi kumi na tano Rajabu.

Mhadhara umetolewa na Shekh Muhsin Asadi, amezungumza vitu vingi kuhusu bibi Hauraa (a.s), na msimamo wake mtukufu pamoja na ushujaa aliokua nao wakati wote wa uhai wake, ulio onekana wazi katika tukio la Karbala na baada ya tukio hilo.

Hali kadhalika ameongea kwa ufupi kuhusu siri ya bibi huyu mtakatifu (a.s) na jihadi yake, kuanzia utoto wake na wakati wa tukio la kuvunjwa mbavu mama yake Zaharaa (a.s) na yaliyo wakuta familia ya Mtume (a.s), miongoni mwa mateso, misiba na kuuwawa kwa baba yake kiongozi wa waumini (a.s), na watu walivyo acha kumnusuru kaka yake Imamu Hassan (a.s) na kifo chake (a.s), hadi katika tukio kubwa la mauaji ya Karbala, na mitihani waliyo pata watu wa nyumba ya Mtume kwa ujumla.

Akazungumza nafasi kubwa ya bibi Zainabu na kifo cha kaka yake katika tukio la Karbala na kuendeleza harakati ya kaka yake Imamu Hussein (a.s) ya kutafuta maelewano hadi kifo chake.

Mhadhara ukahitimishwa kwa kusoma utenzi wa kuomboleza ulio zungumzia kifo chake na vifo vya Maimamu wengine wa Ahlulbait (a.s), kisha akawaombea amani waumini wa taifa hili, na Mwenyezi Mungu mtukufu atupe vazi la afya na atuepushie janga hili la Korona.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: