Ofisi ya Sayyid Sistani inawapa pole watu wa Basra kwa kifo cha Allamah Sayyid Ali Abdulhakim Swafi

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Sayyid Ali Sistani inawapa pole watu wa Basra kwa kifo cha muwakilishi wa Marjaa Dini mkuu katika mji huo Sayyid Ali Sayyid Abdulhakim Swafi, aliye fariki alfajiri ya Jumapili mwezi 15 Rajabu 1442h, sawa na tarehe (28 Februali 2021m).

Lifuatalo ni tamko la pole hiyo
kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu.

(Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea)

Tunatoa pole kwa watu wa Basra tukufu

Amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yenu na rehema zake na baraka zake.

Hakika tumeumizwa sana na taarifa ya kifo cha Sayyid Ali Abdulhakim Swafi (Allah amuweke mahala pema peponi), umri wake wote ameutumia katika kufundisha Dini tukufu na kulea waumini Mwenyezi Mungu ampe malipo mema.

Tunatoa pole kwa watu wa Basra na familia yake tukufu pamoja na waumini mote kwa msiba huu mkubwa, tunamuomba Mwenyezi Mungu amuweke katika rehema zake na amfufue pamoja na Mtume Muhammad na kizazi chake kitakatifu, na aipe subira na uvumilivu familia yake.

Hakuna hila wala nguvu ispokua kwa Mwenyezi Mungu mkuu na mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: