Maahadi ya Quráni tukufu –tawi la Najafu- chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kurudi kwa ufundishaji wa njia ya mtandao kwa kutoa semina za Quráni, kwa kuanza na semina za kuwajengea uwezo walimu wa Maahadi.
Wanafundishwa jinsi ya kutumia mitandao ya kufundishia ukiwemo mtandao wa (google meet), na mawasilino kati ya mwalimu na mwanafunzi wa Maahadi.
Semina hii inatokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Korona hapa Iraq, na kutangazwa kwa marufuku ya kutembea, hivyo Maahadi inalazimika kubadilisha mfumo wa ufundishaji kutoka wa kuhudhuria na kuwa wa masafa (mtandao) kutokana na marufuku ya kutembea iliyo wekwa.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya hutoa mafunzo mbalimbali ya Quráni tukufu kila mwaka, lakini kutokana na mazingira ya mwaka huu na marufuku za kutembea zinazo wekwa kutokana na kujikinga na maambukizi imetoa mafunzo machache.