Maahadi ya Quráni tukufu tawi la Najafu imefanya nadwa ya kielimu chini ya anuani isemayo: (Misingi ya usomaji kwa riwaya ya Hafswa na visomo kumi) mkufunzi alikua Shekh Muhammad Fahami Abdu-Sayyid Usfuur kutoka chuo kikuu cha Al-Azhari Misri.
Nadwa imefanyiwa katika tawi la Maahadi na kufuata taratibu zote za kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona, ilifunguliwa kwa Quráni tukufu iliyo somwa na Ahmadi Zamili, ukafuata ujumbe wa makaribisho kutoka kwa kiongozi wa tawi la Maahadi katika mji wa Najafu Sayyid Muhandi Almayali, amemkaribisha sana mkufunzi aliyekuja kutoka nchini Misri, kisha mtoa mada akawasilisha mada yake, amefafanua aina za usomaji wa visomo kumi kwa waislamu.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya, inafanya harakati mbalimbali za Quráni pamoja na kuchukua tahadhari zote za kujikinga na maambukizi.