Kufanikiwa uwekaji wa mfupa bandia sehemu iliyotoka mfupa

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefanikiwa kuweka mfupa wa bandia sehemu iliyotoka mfupa kwenye kiungo cha mgonjwa kutoka mji wa Nasiyya.

Daktari bingwa wa mifupa katika hospitali hiyo Dokta Mustwafa Walidi amesema kuwa: “Mgonjwa alipigwa risasi kwenye mkono, miezi mitatu iliyopita na kuvunjika pamoja na kupotea sehemu kubwa ya mfupa kwenye mkono wake”.

Akaongeza kuwa: “Upasuaji ulichukua saa tatu, tukaweza kuweka mfupa bandia sehemu iliyokua imetoka mfupa na kufanikiwa kurudisha afya ya mgonjwa”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel inajitahidi kutoa huduma bora daima kwa kutumia vifaa tiba vya kisasa chini ya madaktari bingwa kudoka ndani na nje ya nchi, jambo ambalo limeifanya itoe ushindani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila baada ya muda, sambamba na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hatua tofauti za maradhi yao
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: