Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imefungua semina ya (Saqaa) na (Narjisi) za kufundisha (usomaji wa Quráni na hukumu za usomaji), kwa lengo la kueneza utamaduni wa usomaji wa usomaji wa Quráni kwa makundi tofauti ya wasichana.
Kiongozi wa Maahadi hiyo bibi Manaar Jaburi amesema kuwa: “Semina ya (Saqaa) imesajili mabinti wanaosoma vyuo vikuu na semina ya (Narjisi) imesajili makundi mengine ya wasichana kutoka mikoa tofauti ya Iraq”.
Akasema kuwa: “Janga la Korona linalo sumbua taifa halijazuwia ufundishaji wa Quráni tukufu, kwani Maahadi inatumia mitandao ya kijamii katika ufundishaji wake na kuwasiliana na wanafunzi”.
Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni tukufu tawi la wanawake inalenga kufundisha Quráni kwa wanawake, likiwemo somo la “Maarifa ya Quráni”, na kuchangia katika kuandaa kizazi cha wanawake wasomi wa Quráni wenye uwezo wa kufanya tafiti katika sekta zote za Qur’ani tukufu.