Ugeni kutoka kamati ya maelekezo na msaada umefika katika moja ya vikosi vya Samaraa

Maoni katika picha
Kiongozi wa kamati ya maelekezo na msaada chini ya kitengo cha Dini katika Atabatu Abbasiyya tukufu, Shekh Haidari Aaridhwi amesema kuwa: ujumbe wa kamati yetu umetembelea kikosi cha askari wa Samaraa, kwenye kambi za jeshi la Hashdu-Shaábi katika kitongoji cha Armushiyya pembeni ya mji wa Samaraa, ikiwa ni sehemu za ziara zinazo fanywa na kamati hiyo katika vikosi tofauti, kama sehemu ya kuwatia moyo wapiganaji na kuangalia hali zao, sambamba na kutoa msaada kwa kila anayejitolea kulinda amani ya taifa hili tukufu.

Akafafanua kuwa: “Ugeni umekutana na wapiganaji na kuwafikishia salam na dua kutoka kwa Marjaa Dini mkuu, na kuwaasa washikamane na usia wake, kisha ukakabidhi misaada ya baadhi ya vitu wanavyo hitaji pamoja na zawadi za kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akasisitiza kuwa: “Ujumbe wa kamati hiyo bado unaendelea kutoa misaada mbalimbali kwa wapiganaji wa Hashdu-Shaábi na wa serikali katika maeneo tofauti, chini ya ratiba maalum, utoaji wa misaada unafanywa wakati wote na kwenye mazingira yeyote, kwenye uwanja wa mapambano na baada ya mapambano”.

Wapiganaji wameshukuru sana misaada wanayo pewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, na uwepo wake daima katika uwanja wa vita, au kwenye maeneo yaliyo kombolewa, hakika ziara hizi zinatutia moyo wa kuendelea kuwa ngome madhubuti dhidi ya kila anayetaka kuvunja amani ya taifa hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: