Kuondoa uvimbe katika njia ya sauti

Maoni katika picha
Jopo la madaktari katika hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu limefanikiwa kufanya upasuaji wa kuondoa uvime kwenye njia ya sauti kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka hamsini.

Daktari bingwa wa pua, sikio na koo katika hospitali hiyo Dokta Naadhim Imrani amesema: “Jopo letu la madaktari limefaulu kuondoa uvimbe katika njia ya sauti kwa mgonjwa mwenye umri wa miaka (50)”.

Akabainisha kuwa: “Upasuaji umefanywa kwa kutumia teknolojia ya Lizar”.

Akaongeza kuwa: “Mgonjwa ameteseka kwa muda wa mwaka mzima, baada ya kuja katika hospitali yetu na kufanyiwa vipimo tatizo likajulikana kuwa anauvimbe katika njia ya sauti” ukizingatia kuwa vyumba vyetu vya upasuaji vina vifaa-tiba vya kisasa kikiwemo kifaa cha Lizar ambacho kimetuwezesha kufanya upasuaji huo”.

Akasema kuwa: “Mgonjwa amerudi katika hali ya kawaida baada ya kufanyiwa upasuaji, na amerudi katika familia yake kuendelea na maisha kama kawaida, na sauti inatoka vizuri kama alivyokua zamani kabla ya maradhi”.

Tambua kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hutoa tiba nzuri daima kwa kutumia vifaa vya kisasa na madaktari bingwa kutoka ndani na nje ya nchi jambo ambalo limeiwezesha kutoa upinzani mkubwa katika hospitali za kimataifa.

Kumbuka kuwa hospitali ya rufaa Alkafeel hualika madaktari bingwa kila wakati pamoja na kupokea wagonjwa ambao wapo katika hali tofauti za maradhi yao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: