Jarida hilo linatolewa na kituo cha kiislamu na utafiti wa kimkakati chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kila toleo linakua na tafiti mbalimbali, kwa lengo la kuhakikisha maktaba za kiislamu hazikosi majarida ya kitafiti.
Jarida linakanuni za kuandika tafiti zake na kuzisambaza, kama ifuatavyo:
- 1- Linafuata utaratibu wa sekula katika uandishi na utowaji wa fikra.
- 2- Linajikita katika turathi za Istishraqi na kutotosheka na kuonyesha fikra na kauli.
- 3- Tafiti hukaguliwa na kamati ya majaji.
- 4- Mtafiti hutakiwa kufanya marekebisho atakayo elekezwa na kamati ya majaji.
- 5- Kuchelewa au kuwahishwa kuandikwa kwa utafiti kutategemea kamati ya majaji wala sio jukumu la muandishi.
- 6- Utafiti usiwe umesha wahi kutolewa.
- 7- Jarida linahaki ya kurudia kuandika utafiti katika lugha yake ya asili au iliyotafsiriwa, pekeyake au ndani ya kitabu.
- 8- Mada zitakazo sambazwa hazizingatii ulazima wa maoni ya jarida.
- 9- Kutuma wasifu wa muandishi na harakati zake, pamoja na namba ya simu na barua pepe, kupitia anuani ifuatayo: css@gmail.com