Hatua ya kwanza ya kutibu watoto wenye matatizo maalum

Maoni katika picha
Kamati ya pamoja kati ya kitengo cha malezi na elimu ya juu na hospitali ya rufaa Alkafeel, imetembelea Maahadi Alkafeel ya watoto wanao weza kusoma, kuangalia huduma zinazo tolewa na Maahadi kwa watoto hao.

Ziara hii ni sehemu ya kukamilisha mchakato wa kamati wa kubaini watoto wenye mahitaji maalum katika shule za Al-Ameed.

Tumeongea na kiongozi wa idara ya malezi na elimu ya juu Dokta Imaad Dhwalimi kuhusu ziara hiyo, amesema kuwa: “Ziara hii ni muendelezo wa kikao cha kwanza tulicho fanya katika hospitali ya rufaa Alkafeel wiki iliyo pita, kwa ajili ya kubaini (mahitaji maalum) katika Maahadi ya Alkafeel kwa watoto wenye uwezo wa kusoma, pamoja na kuwatambua wajumbe wa kamati na uzowefu wa Maahadi ya Alkafeel katika misingi ya elimu inayo tumiwa na ngazi za juu”.

Akaongeza kuwa: “Kamati imeangalia namna ya kushirikiana katika kuhudumia watoto wenye tatizo la kuongea, na kuwapeleka hospitali kwa ajili ya kufanyiwa vipimo ja kila mmoja apewe huduma kulingana na hali yake”.

Naye mkuu wa Maahadi ya Alkafeel ya watoto wenye uwezo wa kusoma Ustadhat Sara Hafaar amesema kuwa: “Maahadi huwapima na kuwasomesha watoto wenye uwezo wa kujifunza, kwa kutumia vifaa maalum vinavyo tumika kimataifa, chini ya watumishi wenye uzowefu na weledi mkubwa”.

Akaendelea kusema: “Ziara hii inalenga kuangalia uwezo wa Maahadi na kuangalia namna ya kushirikiana, na kubaini hali ya kila mtoto pamoja na kutoa mafunzo maalum ya kutamka na kuongea kwa kila mtoto kulingana na hali yake”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: