Hivi punde: Tamko la ofisi ya Marjaa Dini mkuu kuhusu kukutana na Papa mkuu wa Vatkan

Maoni katika picha
Asubuhi ya leo siku ya Jumamosi mwezi (21 Rajabu 1442h) sawa na tarehe (6 Machi 2021m), ofisi ya Marjaa Dini mkuu katika mji wa Najafu, imetoa tamko la kukutana na Papa mkuu wa Vatkan, ifuatayo ni nakala ya tamko hilo:

Tamko kutoka ofisi ya Mheshimiwa Marjaa Dini mkuu kuhusu kukutana na Papa mkuu wa Vatikan, Mheshimiwa Sayyid Sistani asubuhi ya leo amekutana na Papa mkuu (Papa Fransis) Papa wa kanisa Katoliki na raisi wa selekali ya Vatkan.

Wameongea kuhusu changamoto za mwanaadamu katika zama hizi, na nafasi ya kumuamini Mwenyezi Mungu mtukufu na ujumbe wake pamoja na kushikamana na misingi ya tabia njema.

Mheshimiwa ameongea kuhusu changamoto iliyopo katika mataifa mbalimbali, dhulma, ukatili, ufakiri, ubaguzi wa kidini, kifikra na kutoweka uadilifu katika jamii, hususan chamgamoto inayo zikumba nchi zetu (za mashariki ya kati), vita, ugaidi, vikwazo vya kiuchumi na mengineyo, bila kusahau mateso makubwa wanayopata raia wa Palestina katika ardhi inayokaliwa kimabavu.

Akaashiria nafasi ya viongozi wakuu wa Dini na kiroho katika kupambana na changamoto hizo, na jukumu la kunasihi pande zinazo gombana, kwa kutumia hekima na kujiebusha na lugha chafu, na kuacha kuweka mbele maslahi yao binafsi badala ya haki ya kuishi kwa uhuru na utulivu, akasisitiza umuhimu wa kuongeza juhudi ya kulingania maelewano na kuishi kwa amani na ushirikiano katika jamii, akahimiza kuheshimu haki za watu na kuheshimiana kwa watu wa fikra tofauti.

Akaongea kuhusu nafasi ya Iraq na historia yake tukufu pamoja na ukarimu wa raia wake wenye mitazamo tofauti, akawaombea kushinda mtihani walionao ndani ya muda mfupi, na akaonyesha matumaini ya wakristo wa taifa hili ya kuishi sawa na raia wengine wa Iraq chini ya misingi ya katiba, akasifu nafasi ya Marjaa Dini mkuu na namna alivyo simama imara kuwahami pamoja na wananchi wengine wote wakati wa vita iliyopita, hususan baada ya miji mingi ya Iraq kuvamiwa na magaidi, waliokuwa wanafanya jinai kubwa zisizo elezeka. Mheshimiwa Papa mkuu na wafuasi wa kanisa Katoliki wakaomba kheri na utulivu kwa binaadamu wote, na akapewa pole ya uchovu wa safari ya kuja Najafu katika ziara hii.

21/ Rajabu/ 1442h

Ofisi ya Sayyid Sistani (d.dh) Najafu Ashrafu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: