Opresheni mpya ya kupuliza dawa katika mkoa wa Baabil

Maoni katika picha
Watumishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji wameanza opresheni mpya ya kupuliza dawa katika mkoa wa Baabil, ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa opresheni kama hizo zilizo fanywa katika mji huo siku za nyuma, kwa ajili ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya Korona.

Msemaji wa kikosi hicho ameripoti kuwa: ofisi yetu ya mkoa wa Baabil imepuliza dawa eneo lote la hospitali ya Nuur kama sehemu ya kuitikia wito wao.

Akaongeza kuwa: tumepuliza vituo vyote, njia, vyumba vya madaktari na watumishi na kumbi za wagonjwa.

Akabainisha kuwa: Mkuu wa hospitali ametoa shukrani nyingi kwa viongozi wa kikosi cha Abbasi (a.s) kutokana na kazi kubwa wanayo fanya ya kupambana na maambukizi ya virusi vya Korona na kulinda afya za wananchi.

Kumbuka kuwa kikosi cha Abbasi (a.s) kiliunda kamati maalum ya kupambana na virusi vya Korona, ambayo imeshapuliza dawa mara nyingi katika miji yenye wakazi wengi, na imefanya kila iwezalo katika kupambana na janga hili, ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha kuosha na kuzika watu waliokufa kwa ugonjwa wa Korona katika mji mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: