Arshu-Tilawah mfumo na ujumbe

Maoni katika picha
Kituo cha miradi ya Quráni chini ya Maahadi ya Quráni tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinaendelea na harakati zake za vikao vya usomaji wa Quráni kila wiki, jioni ya kila siku ya Ijumaa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kupitia matangazo mubashara.

Vikao hivyo vya usomaji wa Quráni kila wiki huhudhuriwa na wasomaji wa Ataba mbili takatufu pamoja na kualika wahadhiri wa mada za Quráni, yote hayo hufanywa chini ya mradi wa Arshu-Tilawah, sambamba na kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi, na hurushwa moja kwa moja na luninga ya Quráni tukufu chini ya chanel za kituo cha Karbala.

Tambua kuwa mradi wa Arshu-Tilawah unalenga kunufaika na vipaji pamoja na uwezo mkubwa wa usomaji wa Quráni uliopo Iraq, na kuudhihirisha katika ulimwengu wa kiislamu.

Kumbuka kuwa Maahadi ya Quráni chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinaadamu katika Atabatu Abbasiyya imezowea kufanya harakati mbalimbali za Quráni kila mwaka, kutokana na mazingira ya mwaka huu imetosheka na kufanya harakati hizi chache.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: