Ofisi ya Sayyid Sistani inatoa pole kwa watu wa Oman

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa Dini mkuu Ayatullahi Udhma Sayyid Ali Husseini Sistani siku ya Jumamosi mwezi (21 Rajabu 1442h) sawa na (7 Machi 2021h) imetoa pole kwa watu wa Oman kwa kifo cha mwanachuoni Sayyid Sharafu bun Ali Mussawi (r.a).. lifuatalo ni tamko la pole hiyo:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu

(Hakika sote ni wa Mwenyezi Mungu na hakika kwake tutarejea)

Tumepokea kwa majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mwanachuoni mtukufu Sayyid Sharafu bun Ali Mussawi (t.a.th), aliyetumia umri wake wote katika kufundisha Dini na kutumikia waumini, tunaipa pole familia yake tukufu na wapenzi wake wote pamoja na kila anayejua utukufu wake miongoni mwa raia wa Oman kwa msiba huu mkubwa.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu amuweke mahala pema peponi na aipe subira na uvumilivu familia yake. Hakuna hila wala nguvu ispokua ni za Mwenyezi Mungu mkuu na mtukufu.

21 Rajabu 1442h
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: