Kuendelea kwa opresheni ya kusaidia familia za watu wenye kipato kidogo

Maoni katika picha
Msafara wa kutoa misaada umewasili katika wilaya ya Musayyib mkoani Baabil, kutokana na marufuku ya kutembea kwa sababu ya kuzuwia maambukizi ya virusi vya Korona, umefanywa na idara ya mkoa wa Bagdad/ Karhka, chini ya ofisi ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya, ukiwa ni sehemu ya opresheni ya Marjaiyyatu-Takaaful.

Kiongozi wa idara Sayyid Qassim Rahimu Maámuri ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Misafara ya idara inaendelea kusaidia familia zenye kipato kidogo, za mafakiri na mayatima ambazo zimeathiriwa na marufuku ya kutembea, imetumia idara zake zote katika kufanikisha hili, ukiwemo msafara huu kutoka mkoa wa Bagdad kitongoji cha Karkha, tumegawa vifurushi vya chakula, nguo na pesa, kazi ya ugawaji imefanywa kwa kushirikiana na idara ya Baabil mashariki”.

Msimamizi wa msafara huo Sayyid Salaam Mussawi amesema kuwa: “Leo tumehudumia idadi kubwa ya familia katika wilaya ya Musayyabu, tumegawa karibu vifurushi vya chakula (75) vilivyo kuwa na chakula kilichoiva na kibichi pamoja na nguo na vitu vingine, kwa lengo la kupunguza ukali wa machungu ya maisha kwa familia hizo, sambamba na kuwapa pesa, huu sio msafara wa mwisho, kuna misafara mingi bado inaendelea katika mikoa mbalimbali, tutaendelea kusaidia familia hizi kadri ya uwezo wetu hadi janga hili litakapoisha”.

Kumbuka kuwa mawakibu zilizo chini ya ustawi wa jamii katika Atabatu Abbasiyya, bado zinaendelea na kazi yake chini ya mradi wa Marjaiyyatu-Takaaful katika mikoa yote, zinafanya misafara kila siku ya kwenda kusaidia familia za mafakiri na mayatima, pamoja na Hashdu-Shaábi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: