Hatua ya pili ya uwekaji marumaru sakafu na ukuta wa sega la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Rais wa kitengo cha miradi ya kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu mhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh amesema kuwa, wameingia hatua ya pili ya kuweka marumaru katika eneo la sega la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) (sehemu ya kushoto ndani ya haram takatifu upande wa Kibla), pamoja na kuendelea na kazi zilizo baki katika hatua ya kwanza, sehemu ya katikati ya ukuta wa haram tukufu na sehemu inayokutana na uwanja wa haram takatifu.

Akaongeza kuwa: “Kazi inaendelea kama ilivyo pangwa kwa namna ambayo haitatizi harakati za mazuwaru pamoja na kazi zingine za kumalizia hatua ya kwanza ya uwekaji wa marumaru, sambamba na kutengeneza shelfu za kuwekea vitabu vya ziara na dua”.

Akaendelea kusema: “Kazi tunazo fanya katika hatua hii zinafanana na tulizofanya katika hatua ya kwanza, hatua ya kwanza ilihusisha ubomoaji wa sakafu ya zamani na kuijenga upya kwa uimara mkubwa pamoja na ukuta wake”.

Kumbuka kuwa mradi wa kuweka marumaru uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni miongoni mwa miradi inayokamilisha kazi zilizo fanywa awali, unafanywa kutokana na kuharibika kwa marumaru za zamani kutokana na ukongwe wake kwani zinazaidi ya miaka (50), hivyo uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukaamua kufanya mradi huu kwa ajili ya kupendezesha sehemu hii takatifu na kuifanya kuwa burudisho la nafsi za mazuwaru watukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: