Kuhitimisha semina iliyo endeshwa kwa njia ya mtandao kwa makundi tofauti ya jamii

Maoni katika picha
Kituo cha Multaqal-Qamaru chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya tukufu kimehitimisha semina zilizo endeshwa kwa njia ya mtandao zikiwa na zaidi ya wanufaika (68) kutoka ndani na nje ya mkoa.

Semina ni moja ya harakati zinazo fanywa na kituo kwa njia ya mtandao katika kipindi hiki, wakati siku za nyuma zilikua zinafanywa kwa washiriki kuhudhuria darasani moja kwa moja, zinalenga kujenga uwelewa wa mambo mbalimbali katika jamii.

Mkuu wa kituo Shekh Haarith Dahi amesema kuwa: “Semina imefanywa kwa muda wa siku tatu kupitia jukwaa la (google meet), na imepata muitikio mkubwa, jumla ya mihadhara mitatu imewasilishwa ikiwa na mada zifuatazo:

  • - Shuhuda za kidini na kukubaliana kwake na mazingira halisi.
  • - Rejea za Dini katika kufanyia kazi hekima na kuondoa vurugu.
  • - Misimamo mikali.. sababu zake na tiba yake.
  • - Rejea za Dini na uwezekano wa kuzifanyia kazi”.

Akamaliza kwa kusema: “Kituo kimeandaa ratiba maalum ya kuendesha semina hizi, kulingana na mazingira ya sasa sambamba na changamoto za kimaadili na kijamii zilizopo”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: