Weusi umetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu

Maoni katika picha
Kesho siku ya Jumatano ni mwezi ishirini na tano Rajabu, siku ya kumbukumbu inayo umiza na kuhuzunisha sana, nayo ni kumbukumbu ya kifo cha Imamu wa saba Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s).

Kutokana na kumbukumbu hiyo Atabatu Abbasiyya tukufu imewekwa mapambo meusi, na alama za huzuni na majonzi, vitambaa vyeusi vilivyo andikwa maneno ya kuomboleza vimewekwa kila sehemu.

Tumeandaa ratiba ya kuomboleza inayo endana na mazingira ya sasa, kuna mambo yatakayo fanywa kwa njia ya mtandao na mengine kwa uhudhuriaji sambamba na kufuata maelekezo ya idara ya afya, kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya kimeweka ratiba ya kupokea mawakibu za kuomboleza zitakazo kuja katika malalo hiyo.

Kumbuka kuwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wanaomboleza msiba huu mwezi (25 Rajabu) siku aliyo uwawa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) kwa sumu aliyopewa na watawala waovu wa zama zake akiwa gerezani.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: