Kazi ya kusafisha eneo la Atabatu takatifu inaendelea

Maoni katika picha
Idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi, yenye jukumu la kusimamia usafi katika eneo la Atabatu Abbasiyya tukufu na kwenye uwanja wa haram takatifu.

Kiongozi wa idara hiyo Muhammad Ahmadi Jawadi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kama kawaida kazi za idara yetu huwa hazisimami, tunasafisha eneo lote linalo zunguka Atabatu Abbasiyya tukufu kila siku, pamoja na barabara zinazo elekea katika haram takatifu sambamba na kusafisha sehemu zingine za Ataba tukufu”.

Akaongeza: “Tunafanya kazi kwa kutumia vifaa vya kitengo cha utumishi, kama vile winchi na vinginevyo”.

Akasisitiza kuwa: “Tunaheshimu na kufanyia kazi maelekezo ya afya yanayo tolewa na Atabatu Abbasiyya tukufu, ikiwa ni pamoja na kuvaa barakoa na kutumia vitakasa mikono wakati wa kufanya kazi hiyo”.

Akasema kuwa: “Watumishi wa idara ya usafi wanafanya kazi saa (24) kila siku, kwa ajili ya kuhakikisha sehemu yote ya Ataba inakuwa safi wakati wote”.

Tambua kuwa idara ya usafi chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu ni miongoni mwa idara muhimu sana, kwani inawajibika kuweka muonekano mzuri na kudumisha usafi maeneo yote ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka kuwa kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa huduma za moja kwa moja kwa mazuwaru, na kinatumia uwezo wake wote kuhakikisha kinatoa huduma bora zaidi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: