Mwezi ishirini na tano Rajabu ni siku aliyo kufa kishahidi Imamu Mussa Alkadhim (a.s), naye ni Imamu wa saba katika Maimamu wa kiislamu baada ya Mtume (s.a.w.w) kutoka katika kizazi kitakatifu, ambao Mtume Mtukufu aliwapa nafasi sawa na Quráni, na akawafanya kuwa kiigizo chema kwa watu wenye akili na meli ya uokovu, amani ya waja na nguzo ya taifa, anatokana na familia ya Mtume, kitovu cha elimu na mashukio ya wahayi na hazina ya elimu ya Mwenyezi Mungu.
Inajulikana kuwa Imamu (a.s) alikufa kishahidi mwaka wa (183h) zikiwa zimebaki siku tano katika mwezi wa Rajabu, na inasemekana alikufa mwaka wa (186h), akiwa na miaka hamsini na tano au hamsini na nne.
Imamu (a.s) alipata mateso makubwa, alifungwa minyororo na kuwekwa kizuwizini, akazuwiwa kuwasiliana na watu, baada ya kupitia unyanyasaji wa aina mbalimbali ndio wakaamua kumuuwa, jukumu hilo akapewa Sindi bun Hashiki, kutokana na uovu wake akakubali kutekeleza jukumu hilo.
Sindi akaweka sumu kali kwenye tende kisha akampa Imamu ale kama futari kwani alikua amefunga, Imamu alikula tende kumi kisha akaacha, Sindi akamuambia endelea kula, Imamu akasema: Inatosha hakika umesha fanikiwa unacho taka.
Baada ya Imamu kula tende zenye sumu muili wake ulianza kudhofika kwa sumu na akawa anasikia maumivu makali hadi akafikia kutoka nafsi yake takatifu na kwenda kwa Mola wake mtukufu, dunia ikajaa giza kwa kumkosa na akhera ikanawilika kwa kumpata.
Amani iwe juu yako ewe mtoto wa Mtume siku uliyo zaliwa na siku uliyo kufa kishahidi na siku utakayo fufuliwa.