Mawakibu zinatoa pole kwa Ataba mbili takatifu

Maoni katika picha
Asubuhi ya mwezi ishirini na tano Rajabu, mawakibu za waombolezaji zimemiminika katika Ataba mbili Husseiniyya na Abbasiyya, kuomboleza kifo cha mtawa wa Aalu-Muhammad Imamu Mussa bun Jafari (a.s), wamekuja kumpa pole Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) huku wakiwa wanatokwa machozi na kujipiga vifua vyao kwa huzuni.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha maadhimisho na mawakibu Husseiniyya bwana Riyaadh, amesema: “Mawakibu zimeanza kumiminika tangu asubuhi ya leo kwa ajili ya kukumbuka na kuomboleza kifo cha Imamu aliye uwawa kwa sumu Mussa Alkadhim (a.s), ambaye tarehe ya kifo chake inasadifu leo, tumeweka ratiba ya kupokea mawakibu hizi, matembezi yao yanaanzia karibu na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wanatembea hadi katika haram yake takatifu na baada ya kumpa mole wanakwenda kumpa pole Imamu Hussein (a.s) wakipita katika uwanja wa katikati ya haram mbili takatifu”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa njia maalum za kupita mawakibu, na sehemu kubwa ya mawakibu hizo ni za watu wa Karbala, pamoja na kuzingatia masharti ya kujikinga na maambukizi, uombolezaji wa msiba huu unafanywa katika mazingira ya pekee kutokana na kuwepo kwa maambukizi ya virusi vya Korona, imebidi kila maukibu ijigawe kwenye vikundi vya watu wachache, na watembee kwa kufuata ratiba na muda bila kusababisha msongamano”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: