Uombolezaji wa kifo cha Imamu Alkadhim ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha Dini imeomboleza kifo cha Imamu Mussa bun Jafari (a.s), ambaye kifo chake kimesadifu siku ya Alkhamisi mwezi ishirini na tano Rajabu, imetoa muhadhara wa kuomboleza ndani ya malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) chini ya uhadhiri wa Shekh Muhammad Kuraitwi.

Mzungumzaji ameeleza mateso mengi aliyopitia Imamu Alkadhim (a.s), na dhulma alizo fanyiwa na watawala waovu wa zama zake, na namna alivyo utumikia uislamu na waislamu, akafanikiwa kueneza elimu na uchamungu katika umma pamoja na kuminywa uhuru wake. Hali kadhalika ameongea kuhusu manyanyaso mbalimbali aliyo fanyiwa Imamu (a.s) ikiwa ni pamoja na kufungwa minyororo, kumzuwia kuwasiliana na watu na maudhi mengine mengi, baada ya manyanyaso hayo, wakaamua kumuua kwa namna isiyokua na mfano.

Mhadhara ukahitimishwa kwa kutaja kifo chake na jinsi ulivyo bebwa muili wake na watu wanne wakauweka juu ya daraja la Bagdad wakasema “huyu Imamu wa Rafidhwa”, kisha wafuasi wake wakachukua muili na kushindikizwa na umati mkubwa hadi kwenye makaburi ya Makuraishi, sehemu ambayo leo inaitwa mji wa Kadhimiyya takatifu kutokana na jina lake tukufu (a.s), hadi leo kaburi lake lipo hapo na hutembelewa na watu wengi ambao huomba shida zao hapo, kwani yeye ni mkidhi haja –kwa idhini ya Mwenyezi Mungu- hatapata hasara atakaeshikamana naye na atapata amani atakae amtegemea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: