Chuo kikuu cha Alkafeel kimefanya majlisi ya kuomboleza

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel chini ya kamati ya malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimefanya majlisi ya kuomboleza kukumbuka kifo cha Imamu Mussa bun Jafari Alkadhim (a.s).

Majlisi hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa Abul-Aswadu Du-uliyyu, imehudhuriwa na wakufunzi na viongozi pamoja na raisi wa chuo Dokta Nurisi Dahani, bila kumsahau mjumbe wa kamati kuu ya uongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu Dokta Abbasi Rashidi Mussawi.

Baada ya kusomwa Quráni ya ufunguzi, ukafuata muhadhara uliotolewa na Shekh Abdullahi Dujaili, akaongelea historia ya Imamu huyu na mateso aliyopewa na watawala waovu wa zama zake, miongoni mwa mateso makubwa aliyo fanyiwa ilikuwa ni kufungwa katika jela ya Bagdad, akasema kuwa pamoja na kufungwa kwa baadhi ya Maimamu (a.s) lakini Imamu Kaadhim alikuwa zaidi yao, alifungwa jela ya ugenini mbali na familia yake na hakuruhusiwa kukutana na mtu yeyote, hakuwa na mtu wa kumtembelea wala kumjulia hali, aliwekwa kwenye jela yenye giza chini ya ardhi (kwenye handaki) akiwa amefungwa minyororo ya chuma iliyo haribu miguu yake, akauwawa kwa sumu ndani ya jela bila kushuhudiwa na mke wala wanae.

Akafafanua kuwa pamoja na mateso aliyopitia Imamu Alkadhim (a.s) katika maisha yake, lakini alifanikiwa kufikisha ujumbe wa baba zake (a.s) ambao ni muendelezo wa ujumbe wa babu yao Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), akahimiza tujifunze kutoka katika mwenendo wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s) na katika nuru ya historia yake na kauli zake pamoja na vitendo vyake, alikuwa ni mtu mwenye subira na kuzuwia hasira.

Akahitimisha mhadhara wa majlisi kwa kusoma tenzi za kuomboleza zilizo taja tukio la kifo chake (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: