Kongamano la kimtandao kuhusu kupewa Utume

Maoni katika picha
Chuo kikuu cha Alkafeel kwa kushirikiana na muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu wa Ulaya kimeandaa kongamano la kimtandao kuhusu kupewa Utume, litakalo fanywa siku ya Jumamosi ya mwezi (28 Rajabu 1442h) sawa na tarehe (13 Machi 2021m) saa nane baada ya Adhuhuri.

Kongamano hilo litafanywa chini ya kauli mbiu isemayo “Hakika wewe uko juu ya tabia njema”, litafunguliwa na ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi na ujumbe kutoka katika uongozi wa chuo, kisha utafuata ujumbe kutoka kwa muwakilishi wa Ataba tukufu wa Ulaya.

Kisha zitaanza kuwasilishwa mada (7) za kongamano kutoka ndani na nje ya Iraq, unaweza kushiriki kwa kujiunga na (Zoom) kupitia link ifuatayo: Alkafeel 91887947665
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: