Dondoo ya kumbukumbu ya siku ya kupewa utume

Maoni katika picha
Mwezi wa Rajabu ni sikukuu kwa mawalii wa Mwenyezi Mungu na waja wema, kwa sababu ni mwezi wa kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu, na unakumbukumbu ya neema ya kupewa utume Muhammad (s.a.w.w) Quráni inasema: “Tajeni neema ya Mwenyezi Mungu kwenu” pia ni mwezi ambao alizaliwa mtu aliyekamilisha Dini na akatimiza neema kiongozi wa waumini Ali (a.s).

Pia kuna siku ya kupewa Utume ambayo kumbukumbu yake ni leo mwezi (ishirini na saba Rajabu), siku tukufu sana nayo ni sikuku kubwa, katika siku kama ya leo Mtume Muhammad (s.a.w.w) aliijiwa na malaika Jibrilu (a.s) akampa ujumbe wa Utume.

Riwaya zinasema kuwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) alipewa utume siku ya Jumatatu mwezi ishirini na saba Rajabu, miaka kumi na tatu kabla ya kuhama Maka, na miaka arubaini baada ya mwaka wa tembo na mwaka wa (610) miladiyya.

Utume ulifungamana na kushushiwa wahyi na malaika Jibrilu (a.s), aliye muambia kuwa Mwenyezi Mungu amemchagua kuwa Mtume, pamoja na kuteremshiwa aya tukufu za Quráni.

Aya alizo teremshiwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na malaika Jibrilu siku hiyo, ni aya tano za mwanzo katika surat Al-A’laq, zisemazo: (Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema mwenye kurehemu. Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye Umba. Ameumba binaadamu kwa tone la damu. Soma na Mola wako mlezi ni karimu kushinda wote. Ambaye amefundisha kwa kalamu. Kamfundisha mtu aliyokuwa hayajui).

Siku hii tukufu huitwa siku ya kupewa utume (mabáthu) nayo ni siku tukufu sana, waislamu wote wanatakiwa kuitukuza na kuiheshimu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: