Shindano la (Mabáthu-Nuur)

Maoni katika picha
Kituo cha utamaduni wa familia katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kimetangaza shindano la wanawake litakalo endeshwa kwa nja ya mtandao, kuhusu siku ya Mabáth tukufu, kwa ajili ya kuangazia yaliyojiri siku hiyo kupitia maswali mbalimbali, shindano hilo limepewa jina la (Mabátu-Nuur).

Mkuu wa kituo bibi Asmahani Ibrahim amesema kuwa: “Hili ni moja ya mashindano mengi yanayo andaliwa na kitengo hiki, kwenye matukio tofauti ya kidini, likiwemo tukio hili, la maadhimisho ya kuzaliwa kwa Nuru na Rehema ya Mwenyezi Mungu pamoja na uongofu mkuu, katika siku ambayo utume ulianza, hakika siku hiyo sio sikukuu ya waislamu peke yake, bali ni kwa binaadamu wote, kwani utume wa Muhammad (s.a.w.w) baraka zake zimeenea kwa walimwengu wote”.

Akaongeza kuwa: “Tumeandaa shindano litakalo endeshwa kwa njia ya mtandao, tutauliza maswali yatakayo jibiwa na washiriki, pia kutakuwa na zawadi kwa washindi watatu wa kwanza, baada ya kupiga kura kama kukiwa na washindi zaidi ya watatu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: