Kutokana na kumbukumbu ya siku ya kupewa Utume, kitengo cha masomo ya Quráni katika chuo kikuu Ummul-Banina (a.s) kwa njia ya mtandao tawi la wanawake, chini ya kitengo cha habari na utamaduni katika Atabatu Abbasiyya kimetangaza kuwa kimeandaa fomu maalum itakayo jazwa na wanafunzi wanaopenda kujiunga na masomo yanayo tarajiwa kuanza mwezi wa Shawwal.
Usajili utafanyika kupitia mtandao kwa link ifuatayo: https://2u.pw/WO60V na utaendelea hadi tarehe (1 Mei 2021m).
Kumbuka kuwa kitengo kimejikita katika kufundisha masomo ya Quráni, na kueneza maarifa ya vizito viwili (Quráni na Ahlulbait –a.s-) kwa njia ya mtandao, kwa masomo ya miaka minne mfululizo, chini ya mfumo wa masomo unaotumika kwenye hauza za Najafu, ulio andaliwa na watu walibobea katika sekta ya Quráni.