Kuanza kwa kongamano la kielimu kuhusu kupewa Utume

Maoni katika picha
Alasiri ya leo siku wa Jumamosi mwezi (28 Rajabu 1442h) sawa na tarehe (13 Machi 2021m) shughuli za kongamano la kielimu linalo endeshwa kwa njia ya mtandao kuhusu kumbukumbu ya kupewa Utume zimeanza, linasimamiwa na chuo kikuu cha Alkafeel kwa kushirikiana na muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika nchi za Ulaya chini ya kauli mbiu isemayo: (Hakika wewe uko juu ya tabia njema).

Baada ya kusoma Quráni ya ufunguzi ukafuata ujumbe kutoka kwa kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, uliotolewa kwaniaba yake na mjumbe wa kamati kuu ya uongozi Dokta Abbasi Rashidi Mussawi. Ukafuatiwa na ujumbe wa chuo kikuu cha Alkafeel ulio wasilishwa na mkuu wa chuo hicho Dokta Nuuris Dahani. Kisha ukafuata ujumbe wa muwakilishi wa Atabatu Abbasiyya katika nchi za ulaya Sayyid Ahmadi Raadhwi Alhusseini.

Halafu ukaanza uwasilishwaji wa mada za kitafiti uliofanywa na wasomi wa hauza na sekula, zikawasilishwa mada mbalimbali kuhusu historia ya Mtume Muhammad (s.a.w.w).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: