Mauwa ya mwezi wa Shabani yamepamba dirisha takatifu

Maoni katika picha
Idara ya miti na mapambo, imelipamba dirisha la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuweka mauwa ya aina mbalimbali, kama sehemu ya kupokea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya (a.s) katika mwezi mtukufu wa Shabani utakao anza kesho siku ya Jumatatu.

Imamu Hussein (a.s) alizaliwa mwezi tatu Shabani, na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) mwezi nne, na mwanae Imamu Sajjaad (a.s) mwezi tano, kisha kumbukumbu ya kuzaliwa muokozi wa binaadamu Imamu wa zama (a.f) mwezi kumi na tano, bila kusahau kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Ali Akbaru mtoto wa Imamu Hussein (a.s) mwezi kumi na moja.

Kiongozi wa shamba boy wa Alkafeel Ustadh Ahmadi Mahmuud Atwiwi ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Mauwa yaliyo wekwa juu ya dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s), yanaonyesha mapenzi ya dhati na uaminifu (ikhlasi), yamewekwa kwa umaridadi mkubwa, yapo zaidi ya mauwa (5000), yamewekwa kupitia chupa maalum za mauwa zilizo wekwa kwenye ufito wa juu ya dirisha tukufu, yamewekwa dawa maalum inayo yawezesha kuendelea kuwa katika ubora wake kwa muda mrefu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: