Muonekano wa shangwe na furaha umetanda katika Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kupokea mwezi wa Mtume (s.a.w.w) mwezi mtukufu wa Shabani, wenye ubora na utukufu mkubwa, unamatukio mazuri yanayo furahisha nyoyo za waumini, walizaliwa maimamu watakatifu katika mwezi huu, alizaliwa Imamu Hussein mtoto wa Ali na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na mtoto wake Imamu Ali bun Hussein (a.s), pia kuna kumbukumbu takatifu ya kuzaliwa Imamu Hujjat bun Hassan Almahadi (a.f) tarehe kumi na tano ya mwezi huu mtukufu.
Kiongozi wa kitengo cha uangalizi wa haram tukufu Ustadh Zainul-Aabidina Quraishi amesema kuwa: “Mwezi huu unautukufu maalum, hivyo watumishi wa kitengo chetu wameweka muonekano wa furaha ndani ya uwanja mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kupokea mwezi mtukufu wa Shabani na kuadhimisha kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya (a.s), tumepamba kuta za Ataba tukufu kwa mauwa yanayo ashiria furaha, kwa nini tusifurahi wakati tunakumbuka kuzaliwa kwa waombezi wetu na meli za uokozi wetu Maimamu waongofu baada ya Mtume (s.a.w.w)”.
Akaongeza kuwa: “Aina mbalimbali za vitambaa tulivyo tumia kupamba tumepewa na idara ya ushonaji katika kitengo cha nadhiri, na vimeandikwa ujumbe unao onyesha utukufu wa matukio hayo, vimeandaliwa vizuri kiasi vinatia furaha katika nyoyo sambamba na kuweka mapambo mbalimbali ya mauwa”.