Walimu wanapewa semina ya jinsi ya kufundisha kwa njia ya mtandao

Maoni katika picha
Kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kinatoa mafunzo ya jinsi ya kufundisha kwa kutumia mtandao, kwa ajili ya kuongeza uwelewa wa kutumia teknolojia hiyo ambayo imekuwa njia mbadala ya ufundishaji katika mazingira ya kuenea kwa maambukizi ya virusi vya Korona.

Tumeongea na Ustadh Ahmadi Hamidi Atwani kiongozi wa kamati kuu ya shule za Al-Ameed, amesema kuwa: “Semina hii ni muendelezo wa utoaji wa masomo ya kuwajengea uwezo walimu wa shule za Al-Ameed waliyo pewa katika mwaka wa masomo uliopita (2019 -2020m) na kuwafanya waendane na maendeleo yaliyopo katika shule zao”.

Akaongeza kuwa: “Mada za semina zimegawika sehemu tatu, sehemu ya kwanza ni uwajibikaji na namma ya kuongeza uwezo, sehemu ya pili ni mikakati ya malezi na utekelezaji wake, sehemu ya tatu ni masomo ya mitandao na namna ya kutumia fursa kwa mwalimu wa shule za Al-Ameed”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: