Uwanja wa katikati ya haram mbili umevaa vazi la Shabani

Maoni katika picha
Mwezi wa Shabani umeingia ukiwa na kumbukumbu tukufu za mazazi mema, na Karbala imejaa furaha kufuatia kungia kwa mwezi huo, uwanja wa katikati ya haram mbili umejaa mapambo kwa ajili ya kuingia mwezi huu mtukufu na kusherehekea kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya, Maimamu watakatifu; Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi na mwanae Sajjaad (a.s) na kuzaliwa kwa Imamu wa zama Hujjat Bun Hassan (a.f).

Kiongozi wa habari katika kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili Ustadh Alaa Imaad Badri Alyaasiriy ameuambia mtandao wa Alkafeel kuwa: “Kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili ni sawa na vitengo vingine vya Ataba tukufu, kimejiandaa kupokea mwezi huu mtukufu, kimeweka mapambo mazuri kila mahala yanayotia furaha, kuanzia uwanja wanao zunguka malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hadi kwenye malalo ya ndugu yake Imamu Abu Abdillahi Hussein (a.s), zimewashwa taa za rangi zinazo ngárisha eneo hilo, pamoja na kuweka vitambaa (30) vilivyo andikwa maneno ya hekima kutoka kwa Maimamu wa Ahlulbait (a.s), yanayo eleza tukio hili na utukufu wa wahusika wake, vimewekwa vizuri kwa umaridadi mkubwa pande zote mbili za uwanja mtukufu kila upande ukiwekwa vitambaa (15) na kwenye nguzo ya mnara wa saa”.

Kumbuka kuwa kitengo kinacho simamia uwanja wa katikati ya haram mbili kimeweka ratiba inayo endana na mazingira ya sasa, na kimejipanga kutoa huduma bora kwa kila atakaekanyaga kwenye uwanja huu mtakatifu, nayo ni sehemu ya juhudi zinazo fanywa na Ataba mbili tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: